politics

Tuesday, 31 March 2015

FAST AND FURIOUS 7-TRAILER

Hii ni moja ya filamu kali ya kimarekani inayo kubadilika pande nyingi za dunia.Japo waigizaji wa filamu hii wamempoteza mmoja wa muigazaji mwenzao karibuni  ila bado wanajitahidi kufanya juu chini ili kuwafurahisha mashabiki zao hivyo wame amua kutoa  filamu nyingine FAST 7 ambayo ita achiwa rasmi tarehe 4 april

GET TO KNOW THIS

Wengi tumekuwa na maswali juu ya jux na vanessa mdee je wapo pamoja au laa! ila hii  ni sauti katika moja ya interview na sudi pata kujua baadhi ya ukweli kuhusu wawili hawa
skiliza alaf majibu utajipa mwenyewe juu ya wawili hawa

Unazipenda Mark X? kama unapesa unaweza kucheki na hii ya 2014.

Ukiitegesha camera kwenye kona mbalimbali za Tanzania lazima jioni itakuletea hesabu kubwa ya picha za Toyota Mark X ambazo ni gari za kifahari kutoka kwa Mjapan

noma sana hii mashine speed 120 kwenye kona

WAZAZI KATIKA SHULE ANAYOSOMA MTOTO WA RAPPER JAY Z NA BEYONNCE,WALALAMIKA

Wazazi katika shule anayosoma mtoto wa beyonce na jay z huko hollywood nchini marekani wamechukizwa na kitendo cha blue ivy kuchukuliwa na kupelekwa na  magari sio chini ya mawili na bodguards kila siku


wazazi wengine wameona iyo ni kero kubwa kwani mtoto huyo anabaki akishangawa na wenzake kila mara anapofika shule

japo shule niya watu wazito ila kwa blue ivy imezidi

JACK'S LETTER

Wakati akiendelea kutumikia kifungo akiwa jela huko Macau, Hong Kong nchini China, modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff  ‘Jack Patrick’ amenena mazito juu ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Juma Khalid ‘Jux’, Vanessa Mdee, Aunt Ezekiel na Moze Iyobo.


BARUA KUTOKA CHINA
Jack aliyekamatwa nchini humo kwa msala wa madawa ya kulevya ‘unga’ mwaka 2013 kisha kufungwa miaka sita kwenye Gereza la Macau, hivi karibuni alilitumia gazeti hili barua nzito akionesha kushtushwa na vitu fulani vya mastaa hao.
MIMBA YA AUNT
Moja kati ya mambo yaliyomshtua Jack ni mimba ya mwigizaji Aunt Ezekiel ambaye ni mke wa mtu, Sunday Demonte anayodaiwa kupachikwa na mcheza shoo wa Diamond, Moze Iyobo.
Hata hivyo, katika skendo hiyo, Jack aliwataka watu wamuache Aunt apumzike kwani mapenzi hayachagui hasa kama ana furaha.


“Nimeshtushwa na udaku special Lol! Sasa Aunt ameamua kutulia na Iyobo…acha apumzike mapenzi hayachagui as long as ndiyo furaha yake, that’s okey,” aliandika Jack.

DIAMOND, ZARI
Mbali na mimba hiyo ya Aunt inayoelekea kuzaa matunda muda si mrefu, modo huyo alionesha kushtushwa na penzi la staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Zari akishangaa ilikuwaje hadi jamaa huyo akaachana na Wema Sepetu kisha kutua kwa mrembo huyo mwenye maskani yake nchini Afrika Kusini na Uganda.
“Heh! Kwani Diamond aliachana na Wema tena?” Alihoji Jack na kuongeza:
“Sasa Zari si anakaa South Africa ‘Sauzi’? Wanaonana vipi na Platnumz? Mh! Wala hawatadumu maana mapenzi ya mbalimbali. Labda kama Nasibu (Diamond Platnumz) atahamia South.

 JUX, VANESSA
Jack alipofika kwenye ishu ya kusalitiwa na staa wa Bongo Fleva, Jux akidaiwa kuwa kwenye malovee na sexy lady wa muziki wa Kizazi Kipya, Vanessa ‘Vee Money’, aliandika ishu hiyo kwa hisia zaidi huku akijilaumu mwenyewe kwa kosa alilofanya.

 Ya Jux na Vanessa nimeamua tu kuyaacha coz nipo jela siwezi kumzuia kufanya lolote then ni makosa yangu yaliyofanya hayo yote kutokea.“Sijui hata kama itakuja kutokea tena kuwa wote tena mimi na yeye, that chapter closed already, nahesabia muda mfupi tu now nitatoka lakini sina chochote cha kufanya nionane naye,” alimalizia kuandika Jack. Jack Patrick alihukumiwa kifungo hicho mwaka jana lakini taarifa zilieleza kuwa endapo ataonesha nidhamu gerezani ataachiwa mapenzi hivyo hatakaa jela miaka yote sita
 

Monday, 30 March 2015

DESMOND

This is  one of the models during apex bash 2014,and everything on him  has been designed by detricia dennis in which everybody made noises as he climbed on the stage