Hii ndoa pia ilishuhudiwa na watoto wao wawili mapacha kama wanavyoonekana kwenye picha pamoja na marafiki wengine wa familia pamoja na ndugu ambao idadi yao inafikia 50.

Mimi Dr. Reginald Mengi naahidi kumpenda Jacqueline Ntuyabaliwe katika shida na raha hadi kifo kitutenganishe
Ilikuwa ni furaha, upendo wa dhati na shangwe pomoni.
Baada ya miaka kadhaa ya uhusiano thabiti na uliokuwa umetawaliwa na
upendo usio kifani, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Limited, Dr. Reginald
Mengi na Miss Tanzania, 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe wamefunga
ndoaWawili hao wamebahatika kupata watoto wawili mapacha pamoja. Watoto
hao wa kiume nao waliungana na wazazi wao kushuhudia wazazi wao
wakibadilisha viapo vya ndoa
Dr. Mengi na mke wake Jacqueline
wakiwa wamewashika mikono watoto wao mapacha wakati wakitembea kwenye
moja ya fukwe za bahari ya Hindi nchini Mauritius ilikofungwa ndoa yao
Kwa mujibu wa watu wao wa karibu waliohudhuria, sherehe hiyo ilitawaliwa na furaha ya hali ya juu.
Kwa mujibu wa watu wao wa karibu waliohudhuria, sherehe hiyo ilitawaliwa na furaha ya hali ya juu.

No comments:
Post a Comment