politics

Wednesday, 29 April 2015

Kingine kikubwa kwenye HEADLINES ni hii stori ya uzinduzi wa Meli kubwa 2 za kivita DAR..


16
Kutoka Dar es Salaam leo April 28  2015 kingine ambacho kimechukua nafasi kubwa kwenye HEADLINES ni hii stori ya uzinduzi wa Meli kubwa mbili za Kivita ambazo zimezinduliwa na Rais Kikwete
Meli zimekabidhiwa kwa Kikosi cha Jeshi la Maji TZ Kigamboni.. Hapa unaweza kuona pichaz kutoka kwenye uzinduzi wa Meli hizo.
15
16
15
255

Meli hizi zitakuwa zikitumiwa kwenye patrol katika eneo la Bahari.

Sunday, 5 April 2015

Serikali ya Kenya yamtambua muuaji

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa wakitoroka shambulio


Serikali ya Kenya imemtambua mmoja ya wapiganaji waliohusika katika mauaji ya chuo kikuu cha Garissa kwamba ni mtoto wa afisa wa serikali.
Msemaji wa wizara ya ndani amesema kuwa Abdirahim Abdullahi ni miongoni mwa watu wanne walioshambulia chuo kikuu cha Garissa siku ya alhamisi na kuwaua watu 148.
Mtu huyo sasa ametambulika kama mwana wa kiume wa Chifu wa eneo la Kazkazini mashariki mwa kenya.

Alidaiwa kutoweka na ilihofiwa kwamba amesafiri nchini Somalia.
Wizara ya ndani inasema kuwa wapiganaji wote waliuawa siku ya alhamisi.
Washukiwa wengine watano wamakamatwa kufikia sasa kwa kuhusishwa na mauaji hayo ambayo ni mabaya zaidi kuwahi kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa Alshabaab.

Saturday, 4 April 2015

Reginald Mengi amefunga ndoa na kyln

Harusi hii ambayo imefungwa kwenye ardhi ya nchi ya Mauritius kwenye mwisho wa mwezi March 2015.
Hii ndoa pia ilishuhudiwa na watoto wao wawili mapacha kama wanavyoonekana kwenye picha pamoja na marafiki wengine wa familia pamoja na ndugu ambao idadi yao inafikia 50.












Mimi Dr. Reginald Mengi naahidi kumpenda Jacqueline Ntuyabaliwe katika shida na raha hadi kifo kitutenganishe
Ilikuwa ni furaha, upendo wa dhati na shangwe pomoni.
Baada ya miaka kadhaa ya uhusiano thabiti na uliokuwa umetawaliwa na upendo usio kifani, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Limited, Dr. Reginald Mengi na Miss Tanzania, 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe wamefunga ndoaWawili hao wamebahatika kupata watoto wawili mapacha pamoja. Watoto hao wa kiume nao waliungana na wazazi wao kushuhudia wazazi wao wakibadilisha viapo vya ndoa
 
 
 
Dr. Mengi na mke wake Jacqueline wakiwa wamewashika mikono watoto wao mapacha wakati wakitembea kwenye moja ya fukwe za bahari ya Hindi nchini Mauritius ilikofungwa ndoa yao
Kwa mujibu wa watu wao wa karibu waliohudhuria, sherehe hiyo ilitawaliwa na furaha ya hali ya juu.
 
 
 
 
 

Thursday, 2 April 2015

Kijana tajiri Afrika ni Mtanzania








Mfanyabiashara maarufu nchini na Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohammed Dewji (pichani) kwa mara ya kwanza ameingia kwenye orodha ya mabilionea 29, akiwa tajiri kijana kuliko wote barani Afrika.


Jarida la Forbes la Marekani limemtaja Dewji (39), katika nafasi ya 24 ya matajiri wa Afrika akiwa na utajiri wa Dola 1.3 bilioni za Marekani (Sh2.34 trilioni) unaotokana na biashara mbalimbali anazozifanya kupitia kampuni yake ya Mohammed Enterprises (Metl Group).“Dewji alibadilisha biashara aliyoanzisha baba yake kutoka uuzaji bidhaa na kuwa na viwanda vya Metl,” inasema sehemu ya habari inayomuhusu bilionea huyo Mtanzania
 
 “Alinunua viwanda vya nguo na mafuta vilivyokuwa vinamilikiwa na Serikali kwa bei ndogo na kuvifanya viwe na faida zaidi kwa kutumia mtindo wa kisasa wa menejimenti,”
 Metl ina viwanda vya kutengeneza nguo na bidhaa nyingine za matumizi ya binadamu vikiwamo vyakula, sabuni na vinywaji. Pia ina mapato yanayozidi Dola 1.4 milioni za Marekani (Sh2.5 trilioni) kwa mwaka

Mmiliki wa Facebook amenunua huu upande wa kisiwa cha Hawaii.

Mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg amenunua sehemu kubwa ya kisiwa cha Hawaii iitwayo Kauai ambayo ni hekari 700 kwa dola za Kimarekani milioni 100 ambapo atakuwa anamiliki eneo kubwa ambalo litaendana na hadhi ya bilionea, jarida la Forbes limeripoti.
Hekari hizo 700 zitajumuisha beach resort, mashamba ya miwa na kilimo hai ambapo kwa sheria za Hawaii beach resort hiyo lazima iachwe wazi kwa matumizi ya jamii kwa sababu kisiwa hiko hakina sheria ya umiliki binafsi wa mchanga.
mark
Kisiwa cha Hawaii
Zuckerberg ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 30 anamiliki dola za Kimarekani billion 33 na anakua ni bilionea wa pili kununua sehemu ya Hawaii.
Mwaka jana mwenyekiti wa Oracle Larry Ellison alinunua upande mzima wa Lanai, Hawaii kwa dola milioni 600 ambapo stori nyingine  zinasema Zuckerbug nae anaweza akawa na nia ya kuanzisha majengo upande huo wa Lanai baada ya kuonekana na mkewe Priscilla Chan kwenye maeneo hayo.
mark1
Mark Zuckerberg na mke wake Priscilla Chan
Haya yatakua maendeleo mengine ya Zuckerberg kwani mwaka 2010 alikodisha jengo lake ambalo lipo karibu na makao makuu  ya office za Faceboook na mwaka uliofata aliongeza makazi yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 7 huko Palo Alto, California, Marekani ambapo pia baada ya muda mfupi alitumia dola milioni 30 kununua nyumba nne ambazo ziliunganishwa na makazi yake ya Palo Alto.
mark3
Nyumba ya Mark Zuckerberg

FLOYD MAYWEATHEER KAMNUNULIA MWANAE WA MIAKA 14 ZAWADI YA GARI

http://i2.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/02/flo1.jpgSasa pamoja na utajiri wa magari aliokuwa nao Mayweather ameamua kumnunulia binti yake wa kike mwenye miaka 14 gari ya kifahari aina ya  Rolls Royce yenye thamani ya dola za Kimarekani laki nne.
fusBinti yake Obi Okeke alifafanua kuwa baba yake alimwita na kumwagizia gari hiyo huku akisema itakuwa ikisimamiwa na mama yake lakini mtoto huyo atakua huru kuitumia wakati wote.
floyd
Mayweather na mtoto wake.

Wednesday, 1 April 2015

MJUE MODEL HUYU

Huyu ni moja kati ya ma models wenye umri mdogo walio shiriki katika moja ya tamasha kubwa mwaka jana 2014  kwenye TUSIIME APEX BASH na aliweza kufanya mambo makubwa kama alivyo andaliwa na designer wake DETRICIA DENNIS

HUYU NDIO MTOTO WA MIAKA 3 ANAYEFANYA MAAJABU YA KUKOKOTOA HESABU MPAKA ZA A-LEVEL

Huyu mtoto ana miaka 3 anaitwa Nice, kwao ni Kiteto kijijini huko Manyara.

Lakini cha ajabu ana uwezo wa kufanya hesabu za Sekondari na nyingine ngumu kwa uwezowa kutisha na kuongea kiingereza fasaha kabisa bila kigugumizi. Ukimuongelesha kiswahi li anakwambia'Please speak english'. Cha kushangaza zaidi ni kwamba tangu azaliwe hajawahi kwenda shule au kuhudhuria darasa la aina yoyote.


Na kama ujuavyo mazingira ya kijiji watu huzungumza lugha ya eneo husika lakini yeye ameweza kuongea kingereza bila kujua wapi amejifunza. na unaambiwa wakati mwingine huwafundisha wanafunzi wa form 1.